27 Machi 2015 - 11:14
Chanjo ya Ebola yaonyesha mafanikio Liberia

Watafiti wamesema kuwa awamu ya pili ya majaribio ya peya mbili za chanjo ya Ebola imefanikiwa nchini Liberia, wakiyasifu matokeo hayo kama hatua muhimu kuelekea kuzuwia mripuko mikubwa ya ugonjwa huo hatari.

Mtafiti mkuu mwenza wa ushirika wa utafiti wa chanjo ya Ebola nchini Liberia Fatorma Bolay, amesema chanjo hizo mbili za majaribio zilizotengenezwa na kampuni za SmithKline, na Merck/NewwLink- zimeonyesha kuwa salama kwa washiriki 600.

Jaribio hilo ndiyo lilikuwa la kwanza la kiwango kikubwa cha chanjo ya majaribio ya Ebola. Tangu mwezi Februari, dozi 2,600 zilijaribiwa kwa wafanyakazi wa afya wa Liberia wanaowahudumia wagonjwa wa Ebola.

Chanjo hiyo sasa itapanuliwa na kuwahusisha karibu watu 30,000 nchini kote Liberia, taifa la Afrika Magharibi lililoathiriwa vibaya zaidi na mripuko huo, ambapo visa 9,602 vimeripotiwa, vikiwemo vifo 4,301 kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.