6 Aprili 2015 - 19:46
Watu 100 wauwawa katika mapambano nchini Yemen

Serikali ya Saudia arabia imeapa kuendeleza mashambulizi makali dhidi ya raia wa Yemen, mpaka wamkubali rais Hadi, ambaye wananchi wa Yemen wanampinga.

Idadi ya watu waliokufa nchini Yemen imefikia watu 100, kutokana na mapigano makali yaliodumu kwa masaa 24 kati ya wanaharakati wa kishia wa Huthi wanaoungwa mkono na wananchi na wapiganaji watiifu kwa rais wa aliyejiuzuru wakishirikiana na wapiganaji wa makundi ya kigaidi ya Al-qaeda na Daesh na kusaidiwa na majeshi ya Saudia arabia nchini Yemen.

Wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada mjini Aden wameonya kuendelea kwa hali kuzorota katika taifa hilo masikini kabisa lililo katika rasi ya Uarabauni na ambapo muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia unafanya mashambulizi ya anga dhidi ya raia na wanaharakati wa kishia wa Huthi wenye kuungwa mkono na Iran.

Wakati huo huo afisa mwandamizi wa Shirika la Msalaba Mwekundu amesema shirika hilo limefanikiwa kupeleka shehena ya madawa katika vituo vya afya vya mji wa kusini mwa Yemen, Aden. Robert Mardin mkuu wa operesheni ya usambazaji wa shirika hilo katika kanda ya  Mashariki ya Kati amesema misafara miwili imekwenda katika wilaya za  Crater na al-Ma'alla. Afisa huyo ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba mji wa Aden hauna watu baada ya kukimbiwa kabisa na wakazi.

Serikali ya Saudia arabia imeapa kuendeleza mashambulizi makali dhidi ya raia wa Yemen, mpaka wamkubali rais Hadi, ambaye wananchi wa Yemen wanampinga.