10 Aprili 2015 - 09:16
 Idadi ya waomba hifadhi yapanda Ulaya

Walinzi wa pwani wa Ugiriki wanasema idadi ya wahamiaji haramu wanaowasili kwa njia ya bahari ilipanda mara tatu ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa 2015

Walinzi wa pwani wa Ugiriki wanasema idadi ya wahamiaji haramu wanaowasili kwa njia ya bahari ilipanda mara tatu ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa 2015. Zaidi ya wakimbizi 10,000 walijaribu kuomba hifadhi barani Ulaya wakilinganishwa na 2,800 ndani ya kipindi kama hicho mwaka jana. Hapo jana pekee, wahamiaji 200 waliokolewa kutoka kisiwa cha Gavdos, kilicho kusini mwa mji wa Crete. Wakimbizi wengi hubahatisha maisha yao kwa kuvuuka Bahari ya Mediterranean, wakikimbia maeneo yenye mizozo Mashariki ya Kati na Afrika.