Umoja wa Ulaya umetenga Euro Milioni tatu za haraka kwa ajili ya kuisaidia Nepal katika kukabiliana na madhara yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi. Fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kununulia maji ya kunywa,dawa na mahema. Msaada huo wa Umoja wa Ulaya ni mbali na ule unaotolewa na kila nchi binafsi ya jumuiya hiyo.
Shirika la misaada la Ujerumani linaloshughulikia mambo ya kiufundi, THW, kama vile ugavi wa maji, pia linapeleka watu wake nchini Nepal. Na nchini Nepal kwenyewe wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imefahamisha kwamba idadi ya watu waliokufa hadi sasa kutokana na maafa ya tetemeko la ardhi imeshavuka 4200.
Watu wengine zaidi ya 8000 wamejeruhiwa.