Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesema anataka kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Rais wa Urusi Vladimir Putin na viongozi kadhaa wa nchi za magharibi huku kukizuka hali tete kati ya Ukraine na Urusi. Rais Putin ameishutumu Ukraine kwa kutumia mbinu za kigaidi kujaribu kuiyumbisha rasi ya Crimea, madai ambayo Ukraine imeyakanusha. Poroshenko amesema amemtaka waziri wake wa mambo ya nje kuandaa mazungumzo kupitia njia ya simu kati yake na Rais wa Urusi na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa, makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk. Mapema hii leo Poroshenko aliliagiza jeshi la nchi hiyo kuwa katika hali ya tahadhari kuu katika eneo la Donbass linalopakana na Crimea kutokana na kuzorota kwa uhusiano kati ya nchi yake na Urusi. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya kikao cha faragha leo kujadili mzozo huo kati ya Ukraine na Urusi.
Mpaka sasa viongozi wa Ukraine wanakosa usingizi kwani wanajua fika kuwa Urusi itatoa jibu kali kufuatia uchokozi huo, lakini hawajui jibu hilo litatioka lini na litakuwa vipi.
Mwisho wa habari/ 291