10 Septemba 2016 - 19:57
Mahujaji 16 wa Misri wafariki nchini Saudi Arabia

Wizara ya afya ya Misri imetangaza kuwa: idadi ya mahujaji waliofariki dunia nchini Saudi Arabia toka kuanza msimu wa Hija wa mwaka huu mpaka sasa yafikia mahujaji 16

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizra ya Afya ya Misri imetangaza kuwa toka kuanza msimu wa Hija wa mwaka huu mpaka sasa mahujaji 16 wamefariki dunia nchini humo.
Shirika la habari la (Almasirah) limetangaza kuwa siku ya Ijumaa iliopita Haji mmoja kutoka Misri amefariki dunia kufuatia ajali ya gari nchini humo, ambapo kwa kufariki haji huyo ndio inafikisha idadi ya waliofariki kuwa ni 16 katika msimu wa Hija ya mwaka huu.
Aidha wizara hiyo ilitangaza kuwa mahujaji wengine 15 wa nchi hiyo wamefariki nchini Saudi Arabia kwa sababu ya matatizo ya kimwili na afya zao.
“Ashraful Arabiy” waziri wa mipango wa Misri ambaye kwa sasa ndio msimamizi mkuu wa masuala ya Hija nchini Misri amesema kuwa: mahujaji walikwenda katika msimu wa Hija mwaka huu ni mahujaji 62 elfu na 511 ambapo mpaka sasa 16 kati yao wamepoteza maisha.
Kwa mujibu wa vielelezo vya gazeti la Al-Akhbari la Lebanon likinukuu kutoka wizara ya afya ya Saudi Arabia limetangaza kuwa: Misri ni nchi ambayo ilipoteza mahujaji wengi katika tukio la Mina liliotokea mwaka jana, kwa maana baada ya Iran Misri ndio inayofuata kwa idadi kubwa ya waliopoteza maisha katika tukio hilo, ama nchi hiyo haijaonyesha hali yeyote yakupinga tukio hilo.

mwisho wa Habari/290