16 Oktoba 2016 - 19:33
Magaidi wa Daesh waanza kukimbia mji wa Musol

Kikundi cha kigaidi cha Daesh chaanza kutorosha majeruhi ya wanamgambo wake katika wilaya ya Musol nchini Iraq

Shirika la Habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Daesh leo Jumamosi kimetoa ruhusa kwa magaidi wake waliokuwa majeruhi kutoka katika mji wa Musol Iraq, kwenda wilaya ya Raqqah nchini Syria, hatua hiyo imechukuliwa katika hali ambayo majeshi ya Iraq yako tayari kuanza mashambulizi yake ya kuikomboa wilaya hiyo ya Musol.
Magaidi wa Daesh hivi sasa wanaendeleza kwa kasi kuchimba barabara za chini ya ardhi ndani ya Musol, barabara ambazo ni kubwa kiasi ambacho wataweza kupita kwa kutumia pikipiki, wakikusudia kutumia barabara hizo kukimbia kwenda maeneo mengine.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh pia kimewaachia huru baadhi ya wafungwa wa Musol ambao walikuwa na makosa madogomadogo kama vile kuvuta sigara, kunyoa ndevu kuvaa mavazi yaliokatazwa ambapo walikamatwa na kufungwa katika jela za magaidi hao.
Wananchi wa wilaya ya Musol leo wameshuhudia mabasi 6 yaliojaa magaidi wa Daesh ambao walikuwa wanaishi katika wilaya hiyo, ambapo pia kulionekana na wanawake na watoto miungoni mwao.
Aidha kikundi cha kigaidi cha Daesh leo pia kimewanyonga magaidi 14 kutoka katika kikundi hicho kwa kosa la kutaka kukimbia katika mji wa Musol, hatimaye kuyongwa katika wilaya hiyo.
Wilaya ya Musol ni makao makuu ya mkoa wa Neniveh ambapo ni miungoni mwa miji na wilaya kubwa nchini Iraq ambayo ilitekwa na magaidi wa Daesh toka miaka miwili iliopita mpaka sasa.
mwisho wa Habari/290