Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Magaidi wanodhaminiwa na Marekani nchini Syria kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syria wamepata pigo kubwa kutoka kwa jeshi la Syria na washirika wake.
Ikumbukwe kuwa Magaidi wanodhaminiwa na Marekani siku chache zilipopita walitumia makombora ya sumu dhidi ya wananchi lakini Marekani na washirika wake wanaodhamini magaidi hao walikaa kimya. Jambo lilipelekea mkubwa wa majeshi ya Urusi kutoa wito kwa magaidi hao wakimbie au wasubiri kipigo kizito.
Leo majeshi ya Syria yakiongozwa na wataalamu wa vita kutoka Iran yamefanya hujuma nzito dhidi ya Magaidi wanodhaminiwa na Marekani na kusababisha vifo vya zaidi ya magaidi 150, na wengine wengi kujeruhiwa huku zana zao za kijeshi zikiwa zimeteketezwa kabisa.
Mwisho wa habari/ 291