23 Februari 2017 - 16:46
Mazungumzo ya amani ya Syria yaanza rasmi Uswisi

Mazungumzo ya amani ya Syria chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa yanaendelea jijini Geneva, miezi kumi baada ya kusambaratika kutokana na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na Saudia kuvunja makubaliano na kuendeleza umwagaji damu.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mazungumzo ya amani ya Syria chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa yanaendelea jijini Geneva, miezi kumi baada ya kusambaratika kutokana na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na Saudia kuvunja makubaliano na kuendeleza umwagaji damu.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura alifanya mikutano tofauti na wawakilishi wa ujumbe wa serikali na upinzani leo asubuhi katika ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Uswisi. Siku moja kabla, Mwanadiplomasia huyo ambaye anatuhumiwa kwa kupendelea upande wa wapinzani alipuuza matumaini ya kupatikana makubaliano ya moja kwa moja katika mazungumzo hayo, lakini pande zote zinafahamu kuwa mienendo nchini Syria imebadilika tangu mazungumzo yaliandaliwa mara ya mwisho Geneva mwezi Aprili.

De Mistura anataka pande zote kujadili uwezekano wa kuundwa serikali ya pamoja ya mpito, katiba mpya na kuandaliwa uchaguzi. Duru za upinzani zimesema mikutano ya kwanza leo ilihusu ufafanuzi wa ajenda halisi ya mazungumzo hayo. Mmoja wa wajumbe wa upinzani Abdulahad Astepho amesema magaidi na wapinzani watakuwa na jukumu kubwa katika duru hii ya mazungumzo.

Mazungumzo ya Geneva yanakuja baada ya mashauriano ya Astana, mji mkuu wa Kazakhstan, ambayo yaliratibiwa kwa kiasi kikubwa na Uturuki, mshirika wa karibu wa magaidii katika vita hivyo vinavyochochewa na mataifa ya nje, na Urusi, ambayo mashambulizi yake ya angani yanawasaidia wanajeshi wa sewrikali ya Rais Bashar al-Assad pamoja na Iran ambayo imetuma wataalamu wake wa vita kuongoza vita vya ardhini dhidi ya magaidi.

Ni duru ya nne ya mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa tangu mapema mwaka jana.

Wakati hayo yakijiri, wanaharakati wameripoti leo kutokea mashambulizi makali katika mji wa kusini wa Daraa baina ya wanajeshi wanaoiunga mkono serikali na makundi ya magaidi yanayoongozwa na kundi la al-Qaeda. Mashirika ya habari ya upinzani pia yameripoti mashambulizi ya anga yaliyofanywa na serikali karibu na eneo la Hama, katikati ya Syria.

Serikali inasisitiza kuwa mpango wa kusitisha mapigano hauyalindi makundi ya kigaidi yenye mafungamano na mtandao wa  al-Qaeda, wakati wapinzani wanaoungwa mkono na Marekani wanasema makubaliano waliyosaini mjini Ankara yanayahusisha makundi hayo.

Mwisho wa habari/ 291