Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Recep Tayyib Erdogan” Rais wa serikali ya Uturuki amesema akiituhumu Iran kuwa, Iran inatumia siasa za kibaguzi na kuzitenga jamii zingine nchini Iraq.
Aidha aliyasema hayo katika hutuba yake alipokuwa akizungumzia mambo mbalimbali nchini humo, na kuashiria tukio la kigaidi la London na kusema kuwa, shambulio la kigaidi liliotokea mjini London ni ishara yakuwa, ugaidi hauna mahala na mipaka, alikadhalika magaidi hawazingatii misngi ya kitabia na mwenendo.
Aliendelea kusema kuwa Uturuki itafanya kura ya maoni kuhusu kubadili katiba ya nchi hiyo mnamo mwezi Aprili mwaka huu, alikadhalika itaitisha kufanya kura za maoni nyingine kuhusu kuingia au kutoingia katika umoja wa Ulaya.
Rais wa Uturuki amebainisha kuwa, subira ya Uturuki katika kukabiliana na mitazamo ya umoja wa Ulaya, inakiwango na mwisho, ammbapo pia amesema haitavumilia kuvunjiwa heshima nchi yake, wananchi wake na wanadeplomasia wa nchi hiyo.
Aidha amesisitiza kuwa viongozi wa nchi za umoja wa Ulaya kama wataendelea kumuita kwa sifa ya Udikteta, naye atawaita wabaguzi na wanyanyasaji.
mwisho/ 290