1 Juni 2017 - 08:56
Majeshi ya kujitolea nchini Iraq yawasili katika mipaka y Syri + picha

Mafanikio makubwa ya kikundi cha majeshi ya kujitolea ya wananchi wa Iraq sehmu za Magharibi mwa mkoa wa Neneveh, hasa maenoe yanayokali na wafuasi wa dini ya Izadi hata kufika katika mji wa Albaaji, uliopo karibu na mipaka ya Syria, ambapo kufuatia ushindi huo kiongozi wa wafuasi wa Dini ya Izadi nchini humo amemshukuru kiongozi mkuu wa Mashia wa Iraq kwa msaada aliotoa katika kukabiliana na magai nchini Iraq huku akiwataka vijana wa kiizadi kujinga na jeshi hilo katika kukabiliana na kikundi cha kigaidi cha Daesh

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: baada ya wiki mbili ya vita kupita katika jangwa liliopo magharibi ya Ninaveh, majeshi ya Iraq yamefanikiwa kufika mwisho wa mpaka wa nchi hiyo na Syria na kukisambaratisha kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Kufika kwa majeshi hayo katika mpaka wa Iraq na Syria ni baada ya kazi kubwa iliofanywa na majeshi hayo kwa muda wa siku 15 ambapo wamesafisha kilometa 1500 za jangwa hilo baada ya mapambano makali yalikuwa baina ya magaidi wengi wa Daesh walikuwa na silaha nzito katika sehemu hiyo.

mwisho/ 290