27 Desemba 2018 - 10:41
Ndege za Israel zashambulia Syria

Inasadikiwa kuwa ndege za kivita za Israel zimevunja sheria za kimataifa na kufyatua makombora kuelekea maeneo ya karibu na mji mkuu wa Syria Damascus, na kulipiga ghala la silaha na kuwajeruhi wanajeshi watatu, hata hivyo mitambo ya Syria imefanikiwa kuzuia asilimia kubwa ya makombora hayo.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Inasadikiwa kuwa ndege za kivita za Israel zimevunja sheria za kimataifa na kufyatua makombora kuelekea maeneo ya karibu na mji mkuu wa Syria Damascus, na kulipiga ghala la silaha na kuwajeruhi wanajeshi watatu, hata hivyo mitambo ya Syria imefanikiwa kuzuia asilimia kubwa ya makombora hayo.

Hivyo makombora ya Israel yalifanikiwa kupiga eneo moja tu katika mashambulizi yake.

Shirika la habari la Lebanon liliripoti kuwa ndege za kivita za Israel ziliruka katika anga ya kusini mwa Lebanon.

Shambulizi hilo ni la kwanza tangu Rais wa Marekani Donald Trump alipotangaza wiki iliyopita kuwa Marekani itawaondoa wanajeshi wake wote 2,000 nchini Syria, hatua ambayo itaacha wazi udhibiti wa upande wa mashariki mwa Syria wenye utajiri wa mafuta ambapo Marekani na washirika wake walikuwa wakijichotea utajiri huo. Mpaka sasa jeshi la Israel halijasema chochote kuhusu mashambulizi hayo.

Mashambulizi hayo yaliyofanywa na Israel yamekuja siku mbili baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kusema kuwa kuondolewa kwa wanajeshi 2,000 wa Marekani kutoka kaskazini mashariki mwa Syria hakutoibadili sera ya Israel ya kuwalenga wanajeshi wa Iran nchini Syria. "Tutaendelea kuchukua hatua dhidi ya jaribio la Iran kuwa na uwepo wake kijeshi nchini Syria, na kama patakuwa na haja, tutatanua shughuli zetu nchini humo". Alisema Netanyahu.

Israel imekuwa ikifanya mashambulizi kadhaa ya angani katika maeneo yanayoshukiwa kuwa ya jeshi la Iran na wapiganaji wa Hezbollah nchini Syria, ambako wanaunga mkono utawala wa Rais Bashar al-Assad.

Hata hivyo, Israel imewekewa kizuizi cha kufanya mashambulizi nchini Syria tangu Oktoba wakati Urusi iliipa Syria mfumo wa ulinzi wa anga aina ya S-300 ambao unayaharibu makombora yanayofyatuliwa na adui. Hilo lilijiri mnamo Septemba 17 wakati ndege ya kijeshi ya Urusi ilipoangushwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria wakati wa shambulizi lililofanywa na Israel.

Tukio hilo lilizusha mvutano kati ya Urusi na Israel, ambazo kawaida huwa na mahusiano mazuri na zina kiwango fulani cha ufahamu kuhusu Syria. Mashambulizi ya anga ya Israel yanachukuliwa na Urusi kuwa yanayoweza kuiyumbisha Syria ambako Urusi inalenga kuuyalinda mafanikio ambayo utawala wa Assad umepata katika vita hivyo vinavyodhaminiwa na Israel, nchi za Magharibi na kushirikiana na nchi za Kiarabu.

Viongozi wa kijeshi wa Iran wamekuwa wakiionya Israel kwamba kila shambulizi ililofanya dhidi ya majeshi ya Iran nchini Syria litakuja na kisasi cha kuumiza.

Kwasasa Israel iko katika hali ngumu kwani imeonekana kuelemewa kila kona, huku majeshi ya Iran yakizidi kujitanua katika mashariki yakati.

Mwisho wa habari / 291