Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema kuwa vikwazo vya vimeufanya mzozo wa Venezuela kuwa mbaya zaidi. Hii ni baada ya Marekani ambayo inasababisha machafuko kuonya kuwa huenda ikatangaza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Rais Nicolas Maduro. Katika ripoti ya Marekani ya kila mwaka kwa Baraza la Haki la Umoja wa Mataifa, Bachelet pia alimshutumu vikali Maduro.
Wavenezuela ambao wanakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na mgogoro mkubwa wa kisiasa unaochochewa na mataifa ya kigeni, wanapambana kupata bidhaa za msingi zikiwemo chakula na madawa. Marekani ambayo inamtambua kiongozi wa upinzani Juan Guaido kuwa kiongozi wa mpito wa nchi hiyo, iliiwekea vikwazo kampuni ya mafuta ya Venezuela mwezi uliopita ili kuiangusha serikali ya nchi hiyo.
Urusi imeionya Marekani isithubutu kuingilia kijeshi Venezuela.
Mwisho wa habari / 291