17 Aprili 2019 - 08:09
 Uhaba wa Mafuta waongezeka nchini Syria

Upungufu wa mafuta kwa sehemu kubwa umesababishwa na vikwazo vya nchi za magharibi ambavyo waliiwekea nchi hiyo ili kumtoa madarakani rais Bashar asad.

Shirika la habari la ABNA: Raia wa Syria walioko katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali ambao wamenusirika na miaka minane ya vita wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa nishati ya mafuta hali inayozorotesha harakati za kimaisha kwenye miji mikubwa.

Upungufu wa mafuta kwa sehemu kubwa umesababishwa na vikwazo vya nchi za magharibi ambavyo waliiwekea nchi hiyo ili kumtoa madarakani rais Bashar asad. Pia imesababishwa na uharibifu uliofanywa na makundi ya wapiganaji na magaidi wanaodhaminiwa na nchi za Magharibi nchini Syria.

Marekani ikishirikiana na nchi zaid ya 60 walipeleka majeshi na kudhamini makundi ya wapinagaji ili kuinagusha serikali ya Syria na kusababisha vita vilivyodumu kwa miaka minane, lakini hawakuweza kuiangusha serikali hiyo baada ya majeshi ya Iran na Urusi kuingilia kati na kuzuia njama mbaya za Marekani na washirika wake.

Mwisho wa habari/ 291