8 Juni 2019 - 05:29
Ripoti: Mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na WhatsApp inachochea ufuska na unyanyasaji wa kijinsia

Utafiti uliofanywa katika nchi 35 na kundi la Fondation Scelles la nchini Ufaransa umeitaja mitandao ya kijamii ya Facebook, Snapchat, WhatsApp, Instagram na Tinder kuwa inachochea ufuska na unyanyasaji wa kijinsia.

(ABNA24.com) Utafiti uliofanywa katika nchi 35 na kundi la Fondation Scelles la nchini Ufaransa umeitaja mitandao ya kijamii ya Facebook, Snapchat, WhatsApp, Instagram na Tinder kuwa inachochea ufuska na unyanyasaji wa kijinsia.

Kundi hilo linaloendesha kampeni ya kupinga ufuska na uasherati, limebainisha kwamba hii leo ufuska unaonekana kuhamia katika mtandao ya kijamii, ambapo walanguzi hutumia mitandao hiyo kuwarubuni wanawake hususan mabinti wadogo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unahusika pakubwa kusimamia programu maalumu za simu kwa ajili ya kueneza ufuska, ambazo hutumika kuwarubuni wanawake katika maeneo mbalimbali ya dunia na kuwaingiza katika biashara hiyo haramu. Nchi nyingine zilizohusishwa na kashfa hiyo ni Zambia ambako inaelezwa kuwa kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaoharibiwa kutokana na aghlabu yao kutumia sana mitandao ya kijamii ya WhatsApp na Facebook.

Kundi hilo linaloendesha kampeni ya kupinga ufuska la nchini Ufaransa, limelaani ongezeko la biashara haramu ya binaadamu katika mitandao na limezitaka nchi mbalimbali duniani kuchukua hatua za kuwatia mbaroni wamiliki wa mitandao hiyo ambao wamekuwa wakificha utambulisho wao kwa jamii. Aidha kundi hilo limewataka watumiaji wa mitandao hiyo kuwa makini ili kujiepusha kurubuniwa na walanguzi wa biashara hiyo.




/129