(ABNA24.com) Abdullah Mosri, mwana wa rais aliyeondolewa madarakani wa Misri, Muhammad Morsi amesema kuwa Rais wa sasa wa nchi hiyo, jenerali mstaafu Abdel Fattah al Sisi ndiye aliyehusika na kifo cha baba yake.
Abdullah Morsi ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twetter kwamba Rais Abdel Fattah al Sisi na maafisa wa serikali yake ndio waliomuua baba yake, Mohammad Morsi.
Rais huyo za zamani wa Misri Jumatatu iliyopita alianguka chini na kupoteza fahami na kisha akaaga dunia alipokuwa mahakamani kusikiliza kesi yake. Baada tu ya kifo hicho, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri ilitangaza hali ya hatari kote nchini humo.
Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa, katika kikao cha kusikiliza kesi yake kilichofanyika tarehe 7 Mei, Muhammad Morsi alisema kuwa maisha yake yalikuwa hatarini. Al Jazeera imeongeza kuwa, rais huyo wa zamani wa Misri aliyepinduliwa na jeshi mwaka 2013 alipitisha karibu nusu saa tangu alipoanguka na kuzimia mahakamani bila ya kuchukuliwa hatua yoyote ya maana ya kumpa huduma ya awali au matibabu.
Rais wa hivi sasa wa Misri Abdel Fattah el Sisi ndiye aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'oa madarakani Muhammad Morsi mwaka 2013.
Shirika la kutetea haki za binadamu ya Human Rights Watch pia limetoa taarifa likitangaza kuwa, serikali iliyofanya mapinduzi ya Abdel Fattah al Sisi ndiyo iliyohusika na kifo cha Morsi. Jumanne iliyopita pia ofisi ya Umoja wa Mataifa ilitilia shaka sababu za kifo cha rais huyo wa zamani wa Misri na kutoa wito wa kufanyika uchunguzi huru kuhusu tukio hilo.
/129
22 Juni 2019 - 06:32
Msimbo wa Habari: 953489
Abdullah Mosri, mwana wa rais aliyeondolewa madarakani wa Misri, Muhammad Morsi amesema kuwa Rais wa sasa wa nchi hiyo, jenerali mstaafu Abdel Fattah al Sisi ndiye aliyehusika na kifo cha baba yake.