(ABNA24.com) Waziri wa Haki za Binaadamu wa Pakistan amekosoa kimya cha baadhi ya nchi za Magharibi kuhusiana na shughuli hatari za nyuklia za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kueleza kwamba, hatua hiyo haikubaliki.
Shireen Mazari ameyasema hayo katika mazungumzo na waandishi wa habari ambapo ameongeza kwamba, siasa za undumakuwili za baadhi ya madola ya dunia katika kuzizuia nchi za Waislamu kustafidi na nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani sambamba na kusalia kimya kuhusu silaha hatari za utawala haramu wa Kizayuni, ni jambo ambalo halikubaliki na ni lazima likomeshwe.
Aidha Waziri wa Haki za Binaadamu nchini Pakistan amefafanua kuwa, Pakistan daima imekuwa ikitaka kuimarishwa amani katika eneo na pia kuzuia mifarakano.
Kadhalika Shireen Mazar ametaka kufanyike mazungumzo ya kiistratijia ya nyuklia kati ya India na Pakistan na ameongeza kwamba, serikali ya Islamabad imekuwa ikitaka kuimarishwa amani ya kudumu katika eneo na kwamba silaha za nyuklia za nchi hiyo ni za kiusalama kikamilifu na zinaendana na viwango vya kimataifa.
/129
20 Julai 2019 - 07:52
Msimbo wa Habari: 962817
Waziri wa Haki za Binaadamu wa Pakistan amekosoa kimya cha baadhi ya nchi za Magharibi kuhusiana na shughuli hatari za nyuklia za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kueleza kwamba, hatua hiyo haikubaliki.