(ABNA24.com) Ali Akbar Salehi amezungumzia kuongezeka nafasi ya nishati ya nyuklia katika kudhamini mahitaji ya umeme ya Iran baada ya kukamilika ujenzi wa kinu cha pili na cha tatu vya atomiki vya Bushehr na kubainisha kuwa: Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa, hadi miaka sita ijayo, kinu cha pili cha Bushehr kitaanza kutumika; na hadi miaka minane ijayo kinu cha tatu cha nishati ya nyuklia nacho pia kitakuwa kiko tayari rasmi kuanza kazi.
Mkuu wa AEOI aidha amebainisha kuwa ukarabati wa tanurinyuklia la Arak unaendelea kwa ushirikiano wa China na Uingereza na akaongeza kuwa: Baada ya kusita kwa miezi kadhaa, timu ya pamoja ya Iran, China na Uingereza inayoshughulikia ukarabati wa tanurinyuklia la Arak imeanza tena kazi ya kulikarabati tanurinyuklia hilo.
Salehi ameashiria pia kutupiliwa mbali madai ya rais wa Marekani Donald Trump yaliyowasilishwa kwenye kikao cha karibuni cha Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na kueleza kuwa: Katika kikao hicho, Marekani ambayo ni mchangiaji mkubwa zaidi wa bajeti ya IAEA ilijikuta imetengwa; na ni utawala wa Kizayuni pekee ndio uliotetea na kuunga mkono madai ya Trump.
Bodi ya Magavana ya IAEA ilifanya kikao maalumu tarehe 10 Julai kwa ombi la Marekani ili kujadili hatua zilizochukuliwa na Iran hivi karibuni za kupunguza utekelezaji wa majukumu yake katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. Hata hivyo kikao hicho kilimalizika bila Marekani kupata tija yoyote na kugeuka uwanja wa kukejeliwa na kukebehiwa Washington na waitifaki wake hususan utawala wa Kizayuni wa Israel.../
/129
27 Julai 2019 - 09:06
Msimbo wa Habari: 964802
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema, ujenzi wa kinu cha pili cha nishati ya atomiki cha Bushehr utaanza mwezi ujao wa Agosti.