(ABNA24.com) Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, chokochoko yoyote ile dhidi ya mipaka ya majini ya Iran itakuwa na matokeo mabaya na machungu kwa wavamizi.
Admeri Alireza Tangsiri, Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema hayo leo katika mkoa wa Khuzestan kusini magharibi mwa Iran mbele ya hadhara kubwa ya mabasiji, wapiganaji na waliojitolea katika kipindi cha vita vya miaka minane vya kujihami kutakatifu vilivyoanzishwa na dikteta wa wakati huo wa Iraq Saddam Hussein dhidi ya taifa hili na kueleza kwamba, wanamaji wa Iran wamejiandaa kikamilifu kukabiliana na hujuma na chokochoko ya aina yoyote ile.
Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, kukamatwa meli ya mafuta ya Uingereza na kutiwa mbaroni wanajeshi wa Marekani katika maji ya Ghuba ya Uajemi ni sehemu ndogo tu ya nguvu na uwezo wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) ambayo ilimtikisa adui.
Admeri Tangsiri ametahadharisha kwamba, endapo maadui watafanya kosa na kufanya hujuma yoyote ile dhidi ya Iran basi watakabiliwa na jibu kali na la haraka la kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH).
/129
30 Septemba 2019 - 07:39
Msimbo wa Habari: 979256
Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, chokochoko yoyote ile dhidi ya mipaka ya majini ya Iran itakuwa na matokeo mabaya na machungu kwa wavamizi.