Pezeshkian amepata ushindi huo baada ya kuzoa kura 16,384,403, huku mpinzani wake Saeed Jalili akipata kura 13,538,179. Zaidi ya watu 30,530,157 walijitokeza kupiga kura.
Rais Bashar al-Assad wa Syria sambamba na kumpongeza Dakta Pezeshkian, Rais mteule wa Iran kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa jana amesema kuwa, ushindi huo ni ishara ya wazi ya imani walionayo wananchi kwake.
Aidha Rais Vladimir Putin katika salamu zake za pongezi kwa Pezeshkian amesema serikali yake itaendeleza himaya, uungaji mkono na ushirikiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Wakati huo huo, Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan amesema serikali yake itashirikiana na serikali yake ijayo na wananchi wa Iran kwa ujumla kwa ajili ya kupanua zaidi ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali.
Rais wa Iraq, Abdul Latif Rashid naye amemtumia ujumbe wa pongezi Rais mteule wa Iran na kusisitiza kwamba, uhusiano wa Tehran na Baghdad umekuwa imara na madhubuti katika miaka yote hii na kwamba, mwenendo wa ushirikiano huo utaendelea kwa misingi ya ushirikiano wa pande mbili na kuamianiana.
Kadhalika, Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz na Mrithi wa Ufalme wa Saudia, Mohammed bin Salman wamemtumia Pezeshkian salamu za pongeza kueleza kuwa, wana matumaini uhusiano na ushirikiano wa Tehran na Riyadh utapanuka na kuimarika zaidi katika kipindi cha urais wa Dakta Pezeshkian.Huku hayo yakiarifiwa, Rais Nocolus Maduro wa Venezuela, kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Yván Gil sambamba na kuipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uchaguzi uliofanikiwa, amewasifu watu wenye busara wa Iran waliohudhuria uchaguzi huo kwa wingi ili kuzuia njama za maadui dhidi ya umoja wao. Rais wa Pakistan, Asif Ali Zardari alikuwa miongoni mwa viongozi wa mwanzo duniani kuipongeza Iran kwa kufanikisha uchaguzi, akibainisha kuwa uchaguzi wa Iran ulikuwa nembo ya wazi ya mshikamano na umoja wa kitaifa.
342/