Main Title

source : Parstoday
Jumanne

9 Julai 2024

16:46:59
1470805

Kanani: Marekani iheshimu demokrasia ya kidini nchini Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja msimamo wa serikali ya Marekani kuhusu uchaguzi kuwa wenye kudhihirisha kiwango cha uingiliaji wa siasa mbovu za nchi hiyo mkabala wa Iran na kusema: Inatarajiwa kuwa Marekani itaheshimu demokrasia ya kidini nchini Iran.

Duru ya pili ya uchaguzi wa 14 wa Rais wa Iran ilifanyika Ijumaa iliyopita. Massoud Pezeshkian amechaguliwa kuwa Rais wa tisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya kuibuka na ushindi wa kura milioni 16 na 384,403 kati ya jumla ya kura milioni 30 na 530,157 zilizopigwa.
Nasser Kanani Chafi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema jana katika mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari hapa Tehran kwamba: Kufanyika uchaguzi wa Rais baada ya kupita karibu siku hamsini tokea kufa shahidi Rais Sayyid Ebrahim Rais wa Iran na kushiriki kwa hamasa wananchi katika uchaguzi huo kunadhihirisha kiwango cha demokrasia ya kidini nchini Iran. Kanani Chafi pai amesema kuhusu ripoti ya kila mwaka ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Marekani kuwa: Wizara ya Mambo ya Nje pia imeandaa ripoti kuhusu mifano ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Marekani; na inatazamiwa kuwa zile nchi zinazodai kuwa zinajaribu kutumia suala la haki za binadamu ili kuingilia masuala ya nchi nyingine zinapasa kwanza kuheshimu haki za msingi za raia wao wenyewe. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa: mazungumzo ya kuondoa vikwazo dhidi ya Iran yanategemea mazungumzo ya pande mbili na Iran itatumia suhula zote katika uwanja huo. Katika sehemu nyingine ya mkutano wake na waandishi wa habari, Nasser Kanani Chafi amesema: Shambulio lolote la utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon litahatarisha usalama na kuyumbisha utulivu wa eneo zima; na dunia inapasa kusimama imara mkabala wa chokochoko za utawala huo. 

342/