Main Title

source : Parstoday
Jumanne

9 Julai 2024

16:47:23
1470807

Ghuba ya Uajemi; nembo ya ukweli wa kihistoria usiokanushika

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akijibu msimamo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kuhusiana kuheshimiwa ardhi yote ya Iran na kutopotoshwa jina la Ghuba ya Uajemi.

Katika barua yake hiyo, Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani vikali na kukadhibisha tuhuma za uwongo na zisizo na msingi dhidi ya mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Iran zilizobainishwa katika kifungu cha 11 cha taarifa ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

Balozi Iravani amezitaja tuhuma hizo dhidi ya Iran kuwa ni uingiliaji wa wazi na usio wa kiadilifu katika masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Barua hiyo ya Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, taarifa iliyotolewa na nchi za Kiarabu dhidi ya Iran si tu kuwa ni kinyume na mwenendo wa ujirani mwema, bali inakiuka wazi kanuni za kimsingi za sheria za kimataifa na mkataba wa Umoja wa Mataifa, hasa kanuni kuhusu haki ya mamlaka ya kujitawala nchi na kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine. Barua ya Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imeendelea kubainisha kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena inasisistiza kuhusu mamlaka yake isiyoweza kukanushwa kuhusu kumiliki kwake visiwa vya Iran vya Bu Musa, Tomb Kubwa na Tomb Ndogo katika Ghuba ya Uajemi.

342/