2 Oktoba 2024 - 18:55
Mufti Mkuu wa Russia ametoa pole kwa kifo cha kishahidi cha Syed Hassan Nasrullah

Mkuu wa idara ya kidini ya Waislamu wa Shirikisho la Urusi na Mufti Mkuu wa nchi hii ametoa salamu za rambirambi kutokana na kuuawa Shahid Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Sheikh Ravil Ainuddin, Mkuu wa utawala wa Kidini wa Waislamu wa Shirikisho la Urusi na Mufti Mkuu wa nchi hii, ametoa salama za rambirambi na maombolezo katika ujumbe wake kuhusiana na Mnasaba wa Kifo cha Kishahidi cha Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon.

Sheikh Ravil Ainuddin aliandika katika ujumbe huu: Kwa niaba ya Idara ya Masuala ya Dini ya Waislamu wa Shirikisho la Urusi na masheikh wa kiroho wa nchi yetu, natoa pole kwa wananchi wa nchi hii kwa kuuawa Shahid Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah, huko Beirut.

Katika ujumbe huu, Mufti Mkuu wa Russia amemuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amjaalie Shahidi Nasrullah kuwa katika daraja za juu za kimungu.

Sheikh Ain al-Din aliendelea na ujumbe huu na kuandika: 

Tunaomboleza mamia ya wahanga wa Lebanon kutokana na mashambulizi ya ndege za kivita za Israel katika siku za hivi karibuni.

Aliongeza kusema: 

Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema azirehemu roho za ndugu zetu ambao ni wahanga wa uvamizi wa Israel na awape malipo mema ya milele.