Mpatanishi Mkuu wa Serikali ya Mamlaka ya Palestina Saeb Erakat amemjia juu Romney ambaye alikuwa nchini Israel na kusema matamshi yake ya kuona serikali ya Jerusalem ni bora kuliko yao ni kitu kibaya sana.
Erakat amekwenda mbali na kuweka bayana matamshi kama haya hayawezi kusaidia mchakato wa kupatikana kwa amani katika eneo la Mashariki ya Kati kama ambavyo juhudi zimekuwa zikifanywa.
Upande mwingine Mgombea huyo mtarajiwa wa Urais kupitia Tiketi ya Chama Cha Repuclican nchini Marekani Mitt Romney amewasili nchini Poland kuendelea na ziara yake katika mataifaya Ulaya huku akitumia sehemu kubwa ya hutoba yake kusifia uchumi wa Taifa hilo.
Romney bila ya wasiwasi wowote amepongeza kwa kiasi kikubwa juhudi ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Viongozi wa Poland katika kuhakikisha uchumi wao unaimarika tangu mwaka jana.
Mgombea huyo Mtarajiwa wa kiti cha urais amekuwa kwenye ziara ambayo inatafsiriwa kama ya kusaka uungwaji mkono na hapa akapata fursa ya kuhutubia wananchi wa Poland waliojitokeza kumsikiliza.