Main Title

source : Pars Today
Jumatatu

17 Juni 2019

10:30:31
952024

Kuhusishwa kundi la Daesh (ISIS), Saudia na Imarati na shambulizi la meli za mafuta

Anthony Cordesman, mchambuzi wa nchini Marekani kuhusu masuala ya Iran amesema kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba tukio la kushambuliwa meli mbili za mafuta za Japan katika Bahari ya Oman, lilifanywa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) kwa ushirikiano na ufadhili wa Saudia na Imarati.

(ABNA24.com) Anthony Cordesman, mchambuzi wa nchini Marekani kuhusu masuala ya Iran amesema kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba tukio la kushambuliwa meli mbili za mafuta za Japan katika Bahari ya Oman, lilifanywa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) kwa ushirikiano na ufadhili wa Saudia na Imarati.

Katika hali ambayo Marekani imetoa video inayoonyesha boti moja inayodai kuwa ni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  na kusema kuwa ndiyo ilihusika kushambulia meli hizo za mafuta siku ya Alkhamisi katika maji ya bahari ya Oman, Anthony Cordesman, mtaalamu huru wa masuala ya kisiasa wa Marekani, sambamba na kutilia shaka video hiyo amezitaja pande zilizohusika na hujuma hiyo. Cordesman anayejishughulisha katika kituo cha utafiti wa kistratijia na kimataifa  cha nchini Marekani ameyasema hayo katika mahojiano na jarida la Newsweek na kubainisha kwamba genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) ndilo lilitekeleza shambulizi hilo ili kuisukuma Washington iishambulie kijeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amezidi kubainisha kwamba Saudia na Imarati ndizo ziliratibu shambulio hilo kwa lengo la kuzidisha mashinikizo dhidi ya Tehran. Aidha jarida hilo la Newsweek limefafanua senario nzima ya shambulizi hilo la siku ya Alkhamisi na kuongeza kwamba, huenda kuna wahusika kadhaa waliohusika na hujuma hiyo. Likizungumzia video iliyotolewa na Marekani na ambayo haipo wazi katika kutoa madai yasiyo na msingi kwamba boti iliyoonekana katika eneo la tukio ni ya Iran, jarida hilo limekadhibisha madai hayo ya Washington. Limesema video hiyo ya Marekani ilitolewa baada ya Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kutoa madai kwamba Iran ndiyo iliyohusika na tukio hilo. Hata hivyo Anthony Cordesman amesisitiza kuwa video hiyo haina ushahidi wowote wa kuitwisha Iran tuhuma za shambulizi hilo, kwani wahusika wa mchezo huo ni pande kadhaa zinazojulikana vizuri.

Katika uwanja huo, baadhi ya weledi wa mambo pia wameashiria kuwa, kuna uwezekano mkubwa mashambulizi ya siku ya Alkhamisi na pia mashambuliai ya mwezi Mei mwaka huu dhidi ya meli nne za mafuta katika bandari ya Fujairah ya Imarati, ni operesheni za 'upeperushaji bendera ghalati' ya utawala wa Kizayuni kwa lengo la kuitia hatiani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kuhusiana na suala hilo George Galloway, mchambuzi mashuhuri wa masuala ya kisiasa na mbunge wa zamani wa Uingereza amezitaja tuhuma za viongozi wa Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya Iran kwamba ni  za kijinga. Akifafanua suala hilo, Galloway amesema: "Iwapo mnaamini kwamba Wairani walizishambulia meli za Japan, tena wakati ambao Abe Shinzō, Waziri Mkuu wa Japan alikuwa mjini Tehran, basi nyinyi si tu kwamba ni wendawazimu wa kuzaliwa, bali ni kondoo mnaoyatumikia majibwa yanayopenda vita." Baadhi ya weledi wa mambo wameelezea pia shambulio hilo kwamba huenda lilifanywa na baadhi ya wanachama wa makundi yenye kufurutu ada ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani, ili kwa njia hiyo kupatikane sababu ya serikali ya Washington kutekeleza hujuma za kijeshi dhidi ya Iran.

Ili kuthibitisha mtazamo huo, Lindsey Graham, seneta wa ngazi ya juu wa chama cha Republican na mkuu wa kamati ya masuala ya mahkama katika bunge la Seneti nchini Marekani, hivi karibuni alitoa pendekezo la kufanyika shambulizi dhidi ya meli na vituo vya kusafishia mafuta vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Akiandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter, Graham alidai kwamba: "Hatuwezi tena kuvumilia, na Marekani inatakiwa kujiandaa kufanya shambulizi dhidi ya meli na hata kama itahitajika, kufanyike shambulio dhidi ya vituo vya kusafishia mafuta vya Iran, ili kuwasababishia hasara kubwa Wairani." Matamshi hayo ya Wamarekani yametolewa katika hali ambayo viongozi wa Iran, sambamba na kulaani vikali shambulizi dhidi ya meli za mafuta katika maji ya Bahari ya Oman, wamepinga pia tuhuma zisizo na msingi wowote za Washington dhidi ya nchi hii. Hii ni kwa kuwa madai hayo yametolewa katika hali ambayo baada ya kujiri tukio la moto kwenye meli hizo mbili za mafuta, kikosi cha utafiti na wokozi cha jeshi la majini na wazamiaji cha Iran kilifika haraka eneo la tukio na kufanikiwa kuwaokoa mabaharia na wahudumu wote wa meli hizo, sambamba na kuwapatia huduma stahiki za matibabu hospitalini.



/129