(ABNA24.com) Rais Rouhani ameyasema hayo leo katika kikao cha tume ya kitaifa ya kudhibiti virusi vya Corona pamoja na wakuu wa mikoa wa nchi nzima kupitia njia ya video ambapo sambamba na kubainisha kwamba ili kuvishinda virusi hatari vya Corona kumeundwa kamati za kijamii za kujitolea katika nyanja zote, ameongeza kwamba kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, Iran imevuka hatua hatari ya ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo.
Kadhalika sambamba na kumpongeza Kiongozi Muadhamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kufuatia kutoa amri ya kuundwa na jeshi la nchi kituo cha afya na tiba amebainisha kuwa, amri hiyo imeisaida sana nchi na raia wa Iran.
Akisisitiza ulazima wa kutekelezwa maelekezo ya kiafya yanayotolewa, Rais Hassan Rouhani amesema kuwa, Jumanne ya kesho wizara zote za Iran kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Tiba ma Mafunzo ya Udaktari zitahusika kuwapima watu viwango vya joto katika barabara zote za nchi hii. Amesisitiza kuwa raia wa Iran na viongozi wa serikali kwa kushirikiana pamoja, watavishinda virusi vya Corona.
...........
340