12 Aprili 2020 - 11:02
Iran yatengeneza kipimo cha haraka cha kinga ya mwili ya corona (antibodi)

Mkuu wa Kituo cha Uhusiano wa Umma na Upashaji Habari cha Wizara ya Afya na Tiba ya Iran amesema kuwa tayari nchi hii iimetengeneza kipimo cha antibodi yaani kinga ya mwili ya Covid-19 na kipimo cha haraka cha corona (rapid test) kwa ajili ya kutambua antibodi.

(ABNA24.com) Dakta Kianush Jahanpur ameandika leo asubuhi katika mtandao wake wa Twitter kwamba kufuatia juhudi chungu nzima na ushiriki wa watafiti wa Kiirani hivi karibuni kipimo hicho cha kutambua kinga ya mwili (antibodi) ya covid-19 na kipimo cha haraka cha corona kitapatikana nchini.

Jahanpur ameongeza kuwa aina hii ya utambuzi wa haraka na wa gharama nafuu utarahisisha kutekelezwa marhala ya mchakato bora wa kutokaribiana katika wiki zijazo. Takwimu zinaonyesha kuwa hadi sasa jumla ya watu elfu 70 na 29 wameambukizwa virusi vya corona hapa nchini na 4,357 wameaga dunia.

Aidha watu zaidi ya milioni moja na 770,000 wameambukizwa corona  na wengine108,338 wameaga dunia kwa ugonjwa huo duniani.  

Wakati huo huo huku idadi ya kesi mpya za ugonjwa wa Covid-19 (corona) ikiendelea kushuka kwa siku kadhaa sasa nchini Iran, hadi kufikia jana mchana watu karibu 42,000 walikuwa wamesharuhusiwa kurudi nyumbani kutoka mahospitalini baada ya kupata nafuu kikamilifu.

.............
340