Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hossam Zaki amesema kuwa Uturuki imejificha nyuma ya Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya kwa shabaha ya kudhamini maslahi yake nchini Libya na kuongeza kuwa, Ankara inataka kutimiza maslahi yake ya kisiasa, kijeshi na kiuchumi.
Uturuki imetangaza rasmi kuiunga mkono na kuisaidia kwa hali na mali Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa inayoongozwa na Fayez Sarraj katika mapambano yake dhidi ya lile linalojiita Jeshi la Taifa la Libya linaloongozwa na jenerali muasi, Khalifa Haftar. Kundi hili la jenerali Haftar linasaidiwa na kuungwa mkono na nchi kama Saudi Arabia, imarati, Misri na Ufaransa.
Tarehe 27 Novemba mwaka jana Uturuki na Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya zilitia saini hati mbili za maelewano ya ushirikiano wa kiusalama na uchoraji wa mipaka ya baharini kuhusu jinsi ya kutafuta na kuchimba mafuta na nishati katika maji ya Bahari ya Mediterania. Hatua hiyo imezikasirisha nchi za Misri, Ugiriki na Cyprus.
Katika wiki za hivi karibuni kundi la Khalifa Haftar limelazimika kuondoka katika maeneo mengi ya kistratijia ya Libya baada ya vipigo mtawala mkabala wa jeshi la Serikali ya Mwafaka wa Kiaifa.
342/