9 Agosti 2020 - 12:11
Shamkhani: Marekani imeshindwa katika sera ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameashiria kujiuzulu mjumbe maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran na kusema: "Stratijia ya Marekani ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran na kuangusha mfumo wa Kiislamu sasa imebadilika na kuwa stratijia ya kuizuia Iran itajirike."

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter  leo Ijumaa, Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameandika: "Brian Hook, mjumbe maalumu wa rais wa Marekani katika masuala ya Iran, sawa na John Bolton, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa katika Ikulu ya White House, alikuwa mtu mwenye misimamo mikali na ya kufurutu ada na mwanachama wa chama cha Republican, na ameondoka White House huku akiwa amefeli katika kazi yake."

Brian Hook alitangaza Alhamisi kuwa amejiuzulu kama mjumbe maalumu wa rais wa Marekani katika masuala ya Iran.

Hook alikuwa maarufu kwa msimamo wake wa kupinga mapatano ya nyuklia ya Iran marufuku kama JCPOA sambamba na kutetea sera za mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran. Weledi wa mambo wanasema sera hizo zimefeli kwani hazijaweza kuishinikiza Iran iketi kwenye meza ya mazungumzo kwa maslahi ya Ikulu ya White House.

342/