Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia Dina Mufti ameashiria muelekeo wa nchi yake wa kutumia njia za amani kutatua mgogoro huo na kuonya kwamba ustahamilivu una mwisho wake.
Akizungumza Jumanne, Mufti amesema majeshi ya Sudan yanajipenyeza zaidi katika eneo linalozozoniwa na nchi hizo mbili la al-Fashqa.
Ameituhumu Sudan kuwa inachochea hali ya mambo huku akisema kuwa Ethiopia inafadhilisha udiplomasia kuliko vita lakini amesema kila kitu kina mwisho wake.
Waziri wa Habari wa Sudan na msemaji wa serikali Faisal Mohamed Saleh ameonya kuwa, nchi yake itajibu uvamizi wowote. Ameitaka Ethiopia kusitisha uhasama wake dhidi ya Sudan na wakulima Wasudan.
Mgogoro baina ya nchi hizo mbili unahusu eneo la kilimo la al-Fashqa, ambalo liko katika mipaka ya kimataifa ya Sudan lakini limekuwa likitumiwa kwa muda mrefu na wakulima Waethiopia
Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan inayatuhumu magenge ya Waethiopia kwa kushambulia eneo la al Fashqa Jumatatu ambapo wanawake watano na mtoto mmoja waliuawa.
Ethiopia inaituhumu Sudan kuwa inatumia fursa ya mgogoro wa Tigray kuchochea uhasama katika eneo la al-Fashqa. Kwa miezi kadhaa sasa jeshi la Ethiopia limekuwa vitani na waasi wa eneo la Tigray kaskaizni mwa nchi hiyo. Nchi hizo mbili aidha zinazozana kufuatia uamuzi wa Ethiopia kujenga bwawa kubwa katika Mto Nile. Misri na Sudan zimeungana kupinga ujenzi wa bwawa hilo.
342/