1 Machi 2021 - 20:43
Adam Schiff: Rais yeyote mwingine asionane na mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia

Mkuu wa Kamati ya Taarifa za Kijasusi ya Baraza la Wawakilishi la Marekani ameelezea kufurahishwa kwake na hatua ya kusambazwa taarifa za kiintelijensia za nchi hiyo kuhusu mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi aliyekuwa akiwakosoa viongozi wa hivi sasa wa Saudi Arabia na kusema kuwa, rais mwingine yoyote hapaswi kuonana na mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Adam Schiff amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na "Yahoo News" na huku akigusia ripoti ya kijasusi ya Marekani kuhusu kuhusika moja kwa moja Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia katika mauaji ya Jamal Khashoggi amesema, mikono ya Bin Salman imejaa damu na yeye ndiye aliyetoa amri moja kwa moja ya imma kukamatwa au kuuawa Khashoggi.

Ameongeza kuwa, si mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia pekee mwenye wajibu wa kubeba jukumu la mauaji ya mwandishi huyo, lakini wote waliohusika katika mauaji hayo na kumkata vipande vipande Jamal Khashoggi ambaye alikuwa mkazi wa Marekani, nao inabidi wafuatiliwe kisheria.

342/