Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Rouhani ameyasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa miradi kadhaa katika sekta za viwanda, turathi za ustawi wa jamii, utamaduni, utalii na sanaa za mikono. Akizindua miradin hiyo kwa njia ya video, Rais Rouhani amesema katika sekta ya chuma kumeshuhudiwa ustawi maradufu katika kipindi cha miaka minane ya serikali yake,
Aidha amesema mwaka mpya wa 1400 Hijria Shamsia utakuwa mwaka ambao Mwenyezi Mungu atalimiminia taifa la Iran neema kubwa na wananchi wa Iran watapata mafanikio makubwa katika makabiliano na janga la corona na pia katika vita vya kichumi.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria miradi ya turathi za utamaduni iliyozinduliwa na kusema turathi za utamaduni ni sekta yenye umuhimu mkubwa.
Aidha amesema katika kipindi cha miaka minane iliyopita sekta ya utalii ya Iran imestawi maradufu lakini kutokana na corona imepungua kutokana na hatua zilizochukuliwa kuzuia kuenea ugonjwa huo. Ameelezea matumaini kuwa mwaka ujao baada ya corona kuangamizwa, sekta ya utalii nchini itaweza kuhuishwa.
Aidha Rais Rouhani amesema Iran itaagiza chanjo ya kutosha ya corona kutoka nchi za kigeni na pia chanjo zilizotengenezwa ndani ya nchi zitaanza kutumika na hivyo janga la corona litaangamizwa na serikali itachukua kila hatua zinazowezekana kufanikisha jambo hilo.
342/