Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo Jumanne wakati wa kikao cha Kamati ya Kuratibu Soko la bidhaa na kuongeza kuwa, watu wote wanajua kwamba tulikuwa kwenye kipindi cha miaka mitatu ya vita vya pande zote na visivyo na kifani vya kiuchumi vilivyoanzishwa na maadui dhidi yetu; na kwamba wanafikra wote maafuru na wakubwa wanakiri kwamba kama vita kama hivyo vya kiuchumi ingeliwekewa nchi nyingine yoyote, basi bila ya shaka yoyote uchumi wake ungelisambaratika kabisa.
Ameongeza kuwa, katika kipindi hiki cha miaka mitatu, taifa letu limevumilia na kuhimili matatizo yote. Hata bidhaa na mahitaji ya kimsingi kabisa ya chakula yalikuwa yamewekewa vikwazo na Marekani. Aibu hii kubwa ya Marekani haijawahi kutokea mfano wake katika historia ya jinai za nchi hiyo na historia ya ugaidi wa kiuchumi duniani.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia pia wimbi la maambukizo ya kirusi cha corona humu nchini kwa zaidi ya mwaka sasa na kuongeza kuwa, baada ya Vita vya Pili vya Dunia, dunia haijawhi kukumbwa na mgogoro kama huu wa COVID-19. Karibu karne moja yaani kuanzia mwaka 1918 na kuendelea, dunia haijawahi kukumbwa na janga kama hili la corona ambalo leo hii limesababisha matatizo makubwa ya kila namna dunia nzima.
342/