Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Licha ya kuwa katika kipindi hiki cha mwaka mmoja juhudi nyingi zimefanywa na mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na harakati za kupinga ubaguzi wa rangi ikiwemo harakati ya 'Roho za Weusi ni Muhimu' (Black Lives Matter), lakini bado tatizo hilo sugu lingali linashuhudiwa kwa wingi nchini humo.
George Floyd Mmarekani mweusi aliuawa kinyama na kwa namna ya kutisha na polisi mmoja mbaguzi wa Marekani aliyekuwa ametulia kabisa na bila ya kuwa na wasiwasi wowote, tarehe 25 Mei mwaka uliopita katika mji wa Minneapolis jimboni Minnesota. Polisi huyo katili alimbinya shingoni Floyd kwa goti lake la mguu na hatimaye kumkatia pumzi bila kujali kilio chake cha kutaka apewe fursa ya kuendelea kupumua. Kusambazwa picha za mauaji hayo ya kutisha kuliibua mshtuko, hasira na malalamiko makubwa katika jamii ya Marekani ambayo ilipinga vikali matukio ya ubaguzi wa rangi dhidi ya jamii za wachaceh na hasa Wamarekani wenye asili ya Afrika na kutaka wahusika wawajibishwe kisheria. Malalamiko na maandamano ya kupinga ubaguzi huo wa rangi ambao umekita mizizi katika jeshi la polisi la Marekani yalibainishwa wazi hasa kupitia harakati ya 'Roho za Weusi ni Muhimu.'
Kwa mfano, Tendayi Achiume, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Ubaguzi wa Rangi alitoa mifano kadhaa ambapo polisi na askari usalama wa Marekani wameua raia wengi weusi bila sababu yoyote muhimu na kusisistiza kuwa hali hiyo ni mgogoro mkubwa nchini Marekani na kutaka hatua za dharura zichukuliwe ili kukabiliana nao.
Kwa mujibu wa takwimu za kuaminika, uwezekano wa polisi ya Marekani kumuua raia mwesui ni mara tatu zaidi kuliko wa kuuawa raia mweupe. Kwa hakika, sehemu kubwa ya vitendo vya ubaguzi wa rangi vinavyofanywa na raia weupe wa Marekani huwakumba raia wa jamii za waliowachache kidini na kirangi na hasa watu weusi, ambapo polisi weupe wabaguzi wa rangi huwa ndio wahalifu wakuu katika uwanja huo.
Justin Feldman, mtaalamu wa masuala ya kijamii anasema: Marekani inashikilia nafasi ya kipekee duniani kati ya nchi zilizoendelea kiviwanda kutokana na mauaji mengi ya ubaguzi wa trangi yanayotekelezwa dhidi ya jamii za waliowachache. Nchi hiyo si tu kwamba inashikilia nafasi ya kwanza duniani kutokana na watu wanaouawa na polisi kwa njia hiyo bali polisi husika huwa hawachukuliwa hatua zozote za kisheria wala kisiasa.
Hali hiyo imepelekea baadhi ya viongozi wa sasa na wa zamani wa Marekani kulalamikia ubaguzi wa rangi uliokithiri nchini humo. Kuhusu suala hilo, Rais Joe Biden wa Marekani alisema karibuni kwamba inasikitisha kuona kuwa nchini humo raia weusi wanabaguliwa sehemu nyingi na hata kupewa adhabu kali zaidi mahakamani, wakilinganishwa na wenzao weupe, kwa kosa la aina moja walilofanya.
Barack Obama, rais wa zamani wa Marekani pia amelalamikia jambo hilo na kusema kuwa ubaguzi wa rangi uko kwenye damu ya baadhi ya Wamarekani. Suala hilo limepata uzingatiaji maalumu nchini humo hasa katika kipindi hiki cha kuenea virusi vya corona duniani. Kuenea virusi hivyo kumeziweka jamii za wachache na wahamiaji katika hali ngumu zaidi ambapo sasa ubaguzi wa rangi dhidi yazo hauonekani tu katika jeshi la polisi bali hata katika utolewaji wa huduma za chanjo ya corona, dawa, matibabu na hata kwenye makaburi ya wafu.
Siku kadhaa zilizopita, tovuti ya Hill ya nchini Marekani iliandika kwamba: Hata kama ubaguzi wa rangi ilioratibiwa kimfumo unaonekana na kukemewa zaidi katika maisha ya kijamii, lakini ubaguzi huo pia unatekelezwa kwa siri katika makaburi ya Marekani.
342/