Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani imesema kuwa, kwa sasa virusi vya corona aina ya Delta ndivyo vinavyosambaa na kuambukizwa kwa kasi kubwa zaidi duniani na kuongeza kuwa, aina hiyo imeshagunduliwa katika nchi zisizopungua 85.
Virusi vya corona aina ya Delta au B 1.617.2 viligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini India.
Hata hivyo ili kuzuia unyanyapaaji wa nchi ambako aina mpya za virusi hivyo vimegunduliwa, Shirika la Afya Duniani limeamua kutumia majina la alama makhsusi za kutambulisha virusi hivyo.
Kwa msingi huo virusi vya corona vilivyogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza vimepewa jina la B.1.1.7 au Alpha na vile vilivyogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini vimebatizwa jina la B.1.351 (Beta).
Hadi sasa zaidi ya watu 3,932,952 wameaga duniani kote duniani kutokana na virusi vya corona.
342/