Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shukrani hizo amezitoa wakati alipoonana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian aliyekuwa ziarani nchini Syria. Ikumbukwe kuwa mapema leo asubuhi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amerejea hapa Tehran akitokea kwenye ziara ya kikazi ya kuzitembelea Iraq na Syria.
Katika mazungumzo yake na Rais Bashar al Assad, Bw. Abdollahian amelipongeza taifa la Syria kwa kuitisha uchaguzi uliofana wa Rais na pia ushindi wa kila namna wa kisiasa wa Syria katika upeo wa kimataifa na amewasilisha salamu za vingozi wa ngazi za juu wa Iran kwa Rais Bashar al Assad na wananchi wa Syria. Pande hizo mbili zimejadiliana pia masuala mbalimbali ya kieneo na kimataifa kikiwemo kikao cha kieneo cha kulisaidia na kuliunga mkono taifa la Iraq.
Kabla ya kuonana na Rais Bashar al Assad, Bw. Abdolahian alikuwa ameonana pia na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Syria, Feisal al Miqdad na kujadiliana naye njia za kuimarisha zaidi na zaidi uhusiano wa pande mbili pamoja na masuala ya kieneo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alielekea nchini Syria jana jioni akitokea Baghdad, mji mkuu wa Iraq.
Ikiwa ni safari yake ya kwanza nje ya Iran tangu ateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amir-Abdollahian juzi Jumamosi alielekea Baghdad Iraq kushiriki katika kikao cha kieneo ya kuliunga mkono na kulisaidia taifa la Iraq.
342/