30 Septemba 2021 - 12:35
China: Tunapinga vikali vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China amesema kuwa, nchi yake inapinga vikali vikwazo vya serikali ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Bi Hua Chunying amesema kuwa, serikali ya China inatangaza wazi kupinga takwa la Marekani kwa Beijing linaloitaka ipunguze ununuzi wake wa nishati ya mafuta ya Iran na kwamba, nchi hiyo inapinga vikali vikwazo vya upande mmoja vya serikali ya Washington.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China amesisitiza kuwa, ushirikiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kwa mujibu wa sheria na kanuni za kimataifa.

Amesema kuwa, China na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima zimekuwa zikiheshimu misingi ya usawa na maslahi ya pande mbili pamoja na ushirikiano wa kibiashara ambao unaufanya kila upande kunufaika sawa bin sawia.

Kadhalika msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China amesisitiza kuwa, azimio lolote lile la Marekani lenye kutaka kuweka vikwazo vya upande mmoja litakabiliwa na upinzani wa Beijing.

Siasa za kindumakuwili za Marekani pamoja na uraibu wake wa kuyawekea vikwazo mataifa mengine ya dunia hasa yasiyokubali kuburuzwa na Washington, zimekuwa zikilalamikiwa kila kona ya duniani.

Alena Douhan, ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hivi karibuni alizuungumzia athari mbaya za vikwazo vya upande mmoja kwa haki za binadamu kusisitiza kuwa, vikwazo vya upande mmoja vya Marekani ni kinyume kabisa cha sheria.

342/