Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Papa Francis ameelezea aibu na fedheha iliyolikumba kanisa hilo pamoja na yeye mwenyewe kutokana na matukio ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto uliofanywa na kanisa nchini Ufaransa.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani ameashiria matukio ya takribani watoto 330,000 walionajisiwa na kunyanyaswa kingono nchini Uufaransa na kusema kuwa, idadi hiyo ni kubwa na kwamba anaelezea masikitiko yake na mateso ambayo wahanga hao wamekuwa nayo.
Papa Francis amewataka maaskofu wote na viongozi wa kidini kuchukua hhatua za lazima na za maana ili kuzuia vitendo kama hivyo visikaririwe tena. Aidha, Papa amewataka Wakatoliki wa Ufaransa kuhakikisha kwamba kanisa linabaki kuwa nyumba salama kwa wote.
Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani amesema hayo baada ya kutolewa ripoti iliyotolewa na jopo huru la uchunguzi inayoeleza kuwa katika kipindi cha miaka 70 iliyopita karibu watoto laki tatu elfu 30 wamefanyiwa ukatili wa kingono katika makanisa Katoliki na taasisi nyingine za kanisa hilo nchini Ufaransa.
Kiongozi wa kamisheni huru ya uchunguzi wa ufuska ndani ya Kanisa Katoliki nchini Ufaransa, Jean-Marc Sauvé siku ya Jumanne aliiambia televisheni ya CNN kwamba makasisi, mapardi, maaskofu na maafisa wa taasisi hiyo ya kidini wamewadhalilisha kingono maelfu ya watoto katika kipindi cha miongo saba iliyopita.
342/