Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Tovuti ya habari ya Hill imeripoti kuwa, kuna maseneta kadhaa ambao hawataki kabisa kusikia Trump anatangaza nia ya kugombea urais kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa urais mwaka 2022, kwa sababu wana hofu kuwa hatua hiyo itafuta matumaini yao ya kushinda tena uchaguzi wa Seneti.
Maseneta hao wa chama cha Republican ambao hawakutaka watajwe majina yao ili waweze kueleza kinagaubaga misimamo yao wamesema, hawataki Trump arudi tena kubeba bendera ya chama hicho.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Echelon Insights, ni asilimia 30 tu ya Warepublican ambao wanapenda rais huyo aliyepita wa Marekani awe mgombea urais katika uchaguzi wa 2024 bila ya kuwa na mshindani ndani ya chama hicho.
Alipouhutubia mkutano wa uchaguzi siku ya Jumamosi katika jimbo la Iowa, Donald Trump alisema, kaulimbiu yake ya uchaguzi kwa mwaka 2024 itakuwa ni "Tunarejesha tena na tena adhama ya Marekani".
Trump ni rais pekee katika historia ya Marekani aliyesailiwa mara mbili kwa lengo la kuuzuliwa, baada ya kukabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka, kukwamisha shughuli za Kongresi na kuchochea wafuasi wake wavamie jengo la bunge hilo katika tukio la tarehe 6 Januari 2020.../
342/