20 Novemba 2021 - 11:53
Sekretarieti ya Kuunga Mkono Intifadha ya Palestian yalaani hatua ya Uingereza dhidi ya HAMAS

Sekretarieti ya Kudumu ya Mkutano wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Intifadha ya Palestina Katika Bunge la Iran imelaani vikali hatua ya serikali ya Uingereza ya kuiweka Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa ya sekretarieti hiyo imeeleza kuwa, hatua hiyo ya Uingereza inakinzana wazi kabisa na haki za binadamu.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Sekretarieti ya Kuunga Mkono Intifadha ya Palestina imesema kuwa, hapana shaka kuwa kitendo hicho cha watu waoga ambacho ni mwendelezo wa usaliti wa Tangazo la Balfour katika fremu ya  kuendelea kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina, kuwafanya wakimbizi mamilioni miongoni mwao na kuwaua maelfu ya wanawake, wanaume na watoto wasio hatia wa Kipalestina.

Kwa upande wake Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) nayo imetoa taarifa ya kulaani uamuzi uliojaa chuki wa serikali ya Uingereza wa kuiweka harakati hiyo katika orodha ya 'makundi ya kigaidi.'

342/