Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Matamshi hayo ya Trump ni sehemu ya mahojiano yake na mwandishi habari wa mtandao wa Kizayuni wa Valla, Barack Ravid, yaliyochapishwa leo Ijumaa.
Katika mahojiano hayo Donald Trump amesema: "Niliibiwa kura katika uchaguzi wa rais uliofanyika hapa nchini kwa sababu ya baadhi ya watu wajinga na dhaifu ambao hawakupamba kwa ajili ya rais."
Rais huyo wa zamani wa Marekani ameongeza: "Hakuna kiongozi wa Marekani aliyemfanyia kazi kumhudumia Netanyahu na Israel kama yeye. Amesema mpango wa "Muamala wa Karne" ulikuwa jambo kubwa na kwamba alifanikisha mpango huo kabla ya uchaguzi wa Israel na kumsaidia sana Benjamin Netanyahu.
Trump ameendelea kumshambulia waziri mkuu wa zamani wa Israel akisema: "Netanyahu alikuwa mtu wa kwanza kumpongeza Joe Biden na kwamba alifanya hivyo kwa njia ya video."
"Lilikuwa kosa kubwa", amesisitiza rais huyo wa zamani wa Marekani na kuongeza: "Tangu wakati huo sijazungumza na Netanyahu. Laana zimshukie! Sitamsamehe."
Katika sehemu nyingine ya mahojiano yake Trump amesema: "Kama nisingekuwa rais wa Marekani, nadhani Israel ingetokomezwa."
Itakumbuka kuwa Donald Trump alikuwa rais wa kwanza wa Marekani kutambua rasmi mji unaokaliwa kwa mabavu wa Quds kuwa mji mkuu wa Utawala haramu wa Israel kinyume kabisa na maazmio yote ya kimataifa. Vilevile alitambua ramsi ardhi iliyovamia na kukaliwa kwa mabavu ya Golan, ambayo ni milki ya Syria, kuwa ni sehemu ya utawala ghasibu wa Israel.
342/