23 Aprili 2022 - 14:27
Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:

Maimamu wa Sala za Ijumaa zilizosaliwa jana kote nchini Iran walisema katika khutba zao kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni mwiba katika macho ya maadui na ni tumaini jema kwa kila Muislamu ulimwenguni.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mwezi Aprili 1979 Imam Khomeini, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitoa amri kwa Baraza la Mapinduzi humu nchini kuasisi rasmi Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kutokana na njama nyingi mno zilizokuwa zinalikabili taifa la Kiislamu la Iran.

Hivi sasa ni wakati wa kuadhimisha mwaka wa kuasisiwa rasmi Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH nchini Iran. Kwa mnasaba huo, maimamu wa Sala za Ijumaa zilizosaliwa jana kote nchini Iran walitumia khutba zao kuzungumzia mengi mazuri yaliyofanywa na jeshi la SEPAH na kusisitiza kuwa, jeshi hilo ni fakhari ya kitaifa kwa Iran likiwa bega kwa bega na vikosi vingine vya ulinzi humu nchini, lakini pia ni tumaini la Waislamu wanaopigania ukombozi katika kona tofauti duniani.

Maimamu hao wa Sala za Ijumaa za jana wametoa mwito pia kwa wananchi wote wa Iran, kwa Waislamu na kila mpenda haki duniani kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Siku ya Kimataifa ya Quds kwa mwaka huu wa 1443 Hijria itakuwa Ijumaa ijayo ya tarehe 29 Aprili 2022.

Itakumbukwa kuwa, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yaani Imam Khomeini MA alifanya ubunifu wa kipekee wa kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ili kuyabakisha hai milele mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Palestina.


342/