Wabunge wa Somalia leo wamemchagua Sheikh Adan Mohamed Nur kuwa spika wao mpya, katika uchaguzi uliocheleweshwa kutokana na kutokubaliana juu ya nani hasa atakuwa kiongozi wa kusimamia usalama wa eneo la kupigia kura.
Sheikh Adan Nur ameibuka na ushindi katika uchaguzi uliosimamiwa na Spika wa mpito Abdisalam Liban Dhabancad. Kuchelewa kwa uchaguzi nchini Somalia kulitokana na vurugu za makundi ya wafuasi wa itikakadi kali na mzozo wa madaraka kati ya rais Mohamed Abdullahi Mohamed na Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble.
Mahasimu hao wa siasa za Somalia, wote wamempogeza spika mpya kupitia kurasa zao za za mtandao wa kijamii wa Twitter.
342/