Akihutubia Taasisi ya Australian Lowy, Zelensky amesema, lazima NATO ihakikishe Moscow haitumii silaha za nyuklia dhidi ya vikosi vya Kiev. Na ili kufanya hivyo, akatoa wito kwa kambi hiyo ya kijeshi inayoongozwa na Marekani na jumuiya ya kimataifa kutangulia kufanya mashambulizi dhidi ya Russia kwa ajili ya kile alichosema "ijue nini cha kutarajia" ikiwa itakuja kuamua kuzitumia silaha za nyuklia.Katika hotuba yake hiyo aliyotoa kwa njia ya intaneti, Zelensky amesema: "NATO ifanye nini? Ondoa uwezekano wa Russia kutumia silaha za nyuklia. Kwa mara nyingine tena natoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, kama ilivyokuwa kabla ya Februari 24: kutangulia kushambulia, ili wao [Russia] wajue kitakachowapata ikiwa watatumia, na si vinginevyo."Ikulu ya Russia, Kremlin imekemea na kulaani pendekezo hilo ililotolewa na rais wa Ukraine.
342/