Uchunguzi huo umefanywa na kituo cha kukusanya maoni ya umma cha Russia ambacho kimesema katika ripoti yake hiyo ya jana kwamba, pamoja na kiwango hicho kikubwa cha umaarufu wa Vladimir Putin nchini Russia, lakini matokeo hayo yanayoenesha kupungua - ingawa kidogo sana; umaarufu wake ikilinganishwa na wiki moja iliyopita.
Kiwango cha kuridhika wananchi wa Russia kwa kazi zinazofanywa na serikali ya Rais Putin pia ni asilimia 48 hivi sasa, kiwango ambacho kinaonesha upungufu wa asilimia 1.1 ikilinganishwa na wiki iliyopita.
Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni aidha yanaonesha kuwa, umaarufu wa Waziri Mkuu wa Russia, Mikhail Vladimirovich Mishustin, kati ya wananchi wa nchi hiyo, ni asilimia 51.6 kiwango ambacho pia kinaonesha kupungua kwa asilimia 1.2 ya umaarufu wake ikilianganishwa na matokeo ya uchunguzi uliopita wa maoni.
Kwa upande wa umaarufu wa wakuu wa vyama vya Russia, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha nchi hiyo, Gennady Andreevich Zyuganov, ndiye anayeendelea kuongoza ikilinganishwa na wakuu wa vyama vingine. Umaarufu wake ni asilimia 30.4 kwa mujibu wa matokeo hayo.
Uchunguzi huo wa maoni ulifanyika baina ya tarehe 21 hadi 27 mwezi ulioisha wa Novemba. Watu 1,600 wanawake kwa wanaume wameshirikishwa kwenye uchunguzi huo wa maoni.
342/