Inadaiwa kuwa Zelensky aliomba hilo huku akitaka kuonekana katika video hiyo akitoa ujumbe wa kuhamasisha amani wakati huu nchi yake ikiwa katika vita na jirani yake Russia.
Taarifa za ndani kutoka baadhi ya vyombo vya habari za michezo zinaeleza kuwa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limemkatalia Zelensky ombi lake hilo pasipo kumpa sababu.
Rais wa Ukraine amekuwa akihutubia kwa njia mbalimbali katika matukio makubwa duniani kuhusu amani ikiwa inatafsiriwa kama ishara ya kuomba uungaji mkono katika vita dhidi ya Russia.
Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema shirikisho hilo la soka duniani limechukua hatua ya kusimamisha baadhi ya "taarifa za kisiasa" nchini Qatar kwa sababu linapaswa "kumzingatia kila mtu."
342/