Seyed Ebrahim Raisi ameyasema hayo katika mkutano na Vyacheslav Valodin, Spika wa Bunge la Russia.Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, Raisi ameeleza kwamba, kutumiwa fursa na uwezo zilionao Tehran na Moscow, mbali na kudhamini maslahi ya nchi mbili, kunaweza pia kudhamini maslahi na manufaa ya kikanda.Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, uhusiano wa kiuchumi wa Tehran na Moscow unaendelea kuimarishwa na kustawishwa na akaongezea kwa kusema, nchi hizo mbili zina uwezo wa kila aina katika nyanja mbalimbali za biashara, nishati, upitishaji bidhaa na usafirishaji, jambo ambalo linaweza kufanyiwa kazi katika uga wa kupanua mashirikiano.
Aidha ameeleza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia utekelezwaji kamili wa makubaliano iliyofikia na Russia na kuongeza kuwa: uwezo zilionao pande mbili unaweza kufaidisha kila upande, na kutumiwa kwake kunaweza kuleta manufaa kwa nchi mbili na kudhamini pia maslahi ya kieneo.
Katika mazungumzo hayo, Spika wa Bunge la Russia, Duma amesema, misimamo ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na kuimarisha uhusiano wa kikanda na wa ujirani inawepesisha kupanuliwa mashirikiano kati ya nchi mbili.Vyacheslav Valodin amesema: Russia pia ina mtazamo na maoni sawa kuhusu kustawishwa kiwango cha ushirikiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kwamba ajenda inayofanyiwa kazi na Moscow inaendana na irada ya viongozi wa nchi mbili ya kustawishwa mashirikiano kwa sura endelevu.../342/