3 Februari 2023 - 12:21
Russia yaitishia Israel iwapo itatuma misaada ya silaha nchini Ukraine

Russia imetishia kulipiza kisasi kijeshi dhidi ya utawala haramu wa Israel iwapo utawala huo utatuma silaha kwa Ukraine, baada ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kusema "anatafakari suala hilo."

Maria Zakharova, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, amesema kuhusu suala la kutuma silaha huko Ukraine kwamba, Moscow haiainisha nchi kulingana na jiografia, akielezea kwamba nchi zote zinazotuma silaha huko Ukraine lazima zielewe kwamba Russia itazitambua silaha hizo kuwa ni shabaha halali ya vikosi vyake vya jeshi.

Jumanne iliyopita Benjamin Netanyahu alisema katika mahojiano yake na televisheni ya CNN ya Marekani kwamba anafikiria kutuma msaada wa kijeshi kwa Ukraine, baada ya Washington kutoa wito wa ushiriki zaidi.

Misimamo ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu vita vya Ukraine na uungaji mkono wake kwa Kiev uliibua mvutano kati ya Tel Aviv na Moscow hadi pale Kremlin ilipoamuru kusimamishwa shughuli za Wakala wa Kiyahudi huko Moscow.

Israel ambayo inatambuliwa kuwa mwana mdekezwa wa Marekani, imekuwa ikiiunga mkono Ukraine kwa tahadhari kubwa ikihofia jibu kali la serikali ya Russia.  

342/