15 Machi 2023 - 19:08
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Wenye chuki dhidi ya Uislamu hawaamini maadili na dini

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Wale wenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu hawaamini maadili yoyote ya kibinadamu na dini za Mwenyezi Mungu.

Serikali za nchi za Magharibi katika miaka ya karibuni zimewaunga mkono na kuwafadhili watu wanaoneza chuki dhidi ya Uislamu ambao wamezivunjia heshima thamani na matukufu ya dini tukufu ya Uislamu na Waislamu. 

kwa sababu hiyo Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana lilipasisha azimio likiitangaza tarehe 15 mwezi Machi kila mwaka kama Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Chuki dhidi ya Uislamu. 

Nasser Kan'ani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametwiti leo kwa kuandika kuwa: "Dini Tukufu ya Uislamu na Mtume wa rehma, Muhammad (S.A.W) alibeba ujumbe wa amani, urafiki na kuishi pamoja kkwa maani wanaadamu wote. 

Kan'ani ameongeza kuwa: Wale wanaoeneza chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu hawaamini thamani na maadili yoyote ya kibinadamu na ya dini za mbinguni bali wanaamini kuwa maslahi yao haramu yamo katika kueneza hitilafu na mifarakano kati ya matabaka mbalimbali ya wanaadamu. 

342/