Rais Vladimir Putin alisema jana katika kikao na wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Russia kwamba: "Mabadiliko ya kimsingi katika maisha ya kimataifa yametulazimisha kufanya marekebisho muhimu katika hati kuu za mipango ya kimkakati ikiwa ni pamoja dhana nzima ya sera ya nje ya Russia inayoweka wazi misingi, majukumu na vipaumbele katika shughuli za kidiplomasia.
Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia pia amesema stratejia mpya ya sera ya kigeni ya nchi hiyo inaruhusu kujumuishwa hatua na radiamali za moja kwa moja na kwa mantiki hii Marekani inatambulishwa kuwa mwasisi na injini kuu ya hatua zinazoipiga vita Russia duniani.
Lavrov ameongeza kuwa, kwa kuzingatia mazingira ya vitisho vya nchi ajinabi, stratejia mpya ya sera ya kigeni ya Russia inasisitiza kuwa kanuni ya mafungamano ya kiusalama inategemea usawa kwa pande zote. Amesisitiza kuwa mkakati mpya wa sera ya kigeni wa Russia unaakisi kimantiki maendeleo ya kimapinduzi katika masuala ya kimataifa.
Toleo la awali la mkakati mpya wa sera ya kigeni ya Russia lilichapishwa mnano Novemba 2016 na kusasishwa miaka iliyofuata.
342/